Mmepeana ahadi ya kukutana na mpenzi ME/KE na mkakubaliana time rasmi ya kukutana mahali hapo. Mpenzi kachelewa kufika je utamsubiri kwa muda gani kabla ya kuamua kuondoka? Utakapoamua kuondoka utampigia simu, kumtumia text message at whatsapp kumfahamisha kwamba umemsubiri hakutokea hivyo umeamua kuondoka?
Mie nitasubiri nusu saa na nikiondoka sitampigia simu, wala kuandika text message au whatsapp kwani tabia za kutoheshimu muda wa mtu mie zinanikera sana. Ukipenda unaweza kuita tabia za kiswahili swahili.
Hilo nalo neno Mkuu, Waafrika wengi hawathamini kabisa muda. Kuchelewa kwao kwa mambo yenye umuhimu mkubwa wanaona ni jambo la kawaida kabisa na wengi wao hawajali hata kuomba samahani kwa kuchelewa.