Asanteni wenyeji wetu kutuhifadhi kwa muda

Tunawashukuru ndugu zetu kwa kutuhifadhi kwa muda ila bado tunatafutana tupo wengi mno; kama mnavyojua ngalawa ikipata dhoruba abiria kila mmoja na lwake; mwenye boya haya; mwenye bakuli haya; mwenye dumu haya; mwenye life jacket sawa ili mradi tu kuokoa maisha yake.

Tunawashukuru. Ngoja nitafute ndugu zangu akina Mshana; Mwifwa; Pasco; kina Mzizi mkavu na wengine wengi. pia lile jukwaa letu la mambo ya wakubwa duh sijui itakuwaje.

Hata hivyo tumefundishwa ukikaribishwa kwa mtu don’t ask for more - mwenyeji wako atakuchoka fasta.

@Fuso mimi niliumwa siku hizi mbili baada ya kuona kiza kimetanda kule JF. Nashukuru ndugu zetu kwa kutuazima mkeka huu hapo tulaze ubavu.

Ha ha ha kweli aisee maana

[quote=“Fuso, post:1, topic:163311”]

Tunawashukuru ndugu zetu kwa kutuhifadhi kwa muda ila bado tunafutana tupo wengi mno; kama mnavyojua ngalawa ikipata dhoruba abiria kila mmoja na lwake; mwenye boya haya; mwenye bakuli haya; mwenye dumu haya; mwenye life jacket sawa ili mradi tu kuokoa maisha yake.

Tunawashukuru. Ngoja nitafute ndugu zangu akina Mshana; Mwifwa; Pasco kima Mzizi mkavu; pia lile jukwaa letu la mambo ya wakubwa duh sijui itakuwaje.
[/QUOTE

Ha ha ha hata raha sikuwa nayo kikweli[/QUOTE]

Aisee itachukua muda saana kukutana wote humu; hii ni dhoruba kali. Maisha ni magumu mno kwa sasa chief.

Serikali yetu ime tufanyia kitu mbaya sana ukatili wa hali ya juu

Hawajui nguvu ya Tech; huwezi zuia hata mwanao kutopata info kwenye mitandao eti kisa ataharibika; yaani hata kama umemzaa mwenyewe utakuwa unapoteza muda. Utakuwa baba mjinga saana.

Kaka wacha tujibanze banze si unajua tena mambo ya ugenini…huwezi kujimwaya utakavyo…unaweza kuambiwa kulala saa mbili kamili ha ha ha

I’m just thinking if JF Tanzania can upload data to this portal.

Najua kuna mambo mengi mno watahitaji kukubaliana; ila mambo yote yanawezekana kwenye IT; kiasi kwamba user wote waingie na ID zao za TZ.

Ni ombi tu lakini kwa Mods wa pande zote mbili.

ha hahaaa ata kama ugenini hatulali sa mbili

Kweli Mkuu, hii inaweza kuwameza wakenya wote…

:p:p:p:p:p:p:p:p:p
Tunasubiri wenyeji walale kwanza, maana kulala ni sebuleni

:D:D:D:D:Dacha tuuu

Lazima tukubaliane na hali ya ugenini bana

acha tu asee, nimeteseka sana baada ya dhoruba ile, ila nashukuru tumepata nafasi kwa jirani

Dah ila JF acha tu

TZ ni mziki mnene wanaujua

Kaka si unajua sheria za kulala sebureni, wa mwisho kulala, hadi wenyeji wamalize kuangalia tamthiliya; then wa kwanza kuamka kabla hawajaanza kudeki; maisha ya ugenini yanahitaji uvumilivu mkuu

:p:p:p:p:p:p:p:p

Mumuambie Jiwe aache ujinga sio mnakuja kulalamika kinafiki huku

Jiwe ashaiifanya TZ yote ni chato