Najua ndugu zangu tupo hapa Ugenini, japo hatujajua ni kwa muda tu kisha tutarudi nyumbani au ndio tutakuwa hapa daima.
Nimejaribu kutafuta wataalam wa tiba asili, mambo yakichawi, na mada moto moto za aina hiyo lakini sijawapata kwa hapa Kenya japo kwa tuliotoka pale mjini Jf Tanzania tulikuwa na mtaalamu wetu wa mambo hayo Bw.Mshana Jr.
Najua taarifa za kwamba wenzie tupo huku anazo ila labda anasubiri kuona watu kama watamuulizia na kuhitaji uwepo wake ndipo aamue kuja, sasa kwa andiko hili kama kuna mtu yupo nae karibu basi amwambie tumeanza kumuulizia huku aje haraka, msaidizi wake Mimi wa kilinge sina nguvu sana kwenye uchawi.