Kiswahili endelevu

Ni Siku nyingine njema tuliyojaliwa mabingwa kuweza kupashana makali kwenye hino lugha tuipendayo. Karibuni nyote.

MISAMIATI YA LEO
-Petition.….Aridhihali
-Hermoprodite…huntha
-Nun/Monk…Mtawa
-Teachers staff room…Majilisi
-Office messenger…Tarishi
-Parliamentary Bill…Hoja au Mswada

CHEMSHA BONGO
-Andika majina sahihi ya maelezo yafuatayo;
i) Aina ya kofia yenye sehemu inayotokelezea mbele(cap) huitwa…
ii) Aina ya kizibo cha kufungia na kufungulia maji huitwa…
iii) Mahali maalum palipochimbwa ukutani ili kuhifadhia nguo ni…
iv) Kiti cha kukalia chenye miguu mitatu na kisichokuwa na kiegemeo huitwa…
v) Kifaa maalum kwa ajili ya kuleta ubaridi wakati wa joto(fan) huitwa…
vi) Bainisha kati salamu za Masalkheri na Sabalkheri.
vi) Ukisalimiwa Masalkheri au Sabalkheri, mtu hujibu…
vi) Air conditioner kwa kiswahili ni…
vi) Carpet kwa kiswahili ni…

vii) Bill of exchange/Treasury bills kwa kiswahili ni…

Shukran.Kumbuka Maskini hachoki kutafuta; akichoka, amepata!

Wacha nipige ripoti kwenye ukumbi wa kiswahili…
vi) Air conditioner kwa kiswahili ni… Kiyoyozi.

Leo naona umebisha kwa fujo kaka.

carpet = mkeka

na jee, cockroach huitwaje kwa kiswahili?

HII NINAJUA…HII NINAJUA. Kombamwiko

Fixed

I don’t think so. Na curtain je itaitwa aje?

Pazia

Typing everything in bold huitwa?

Kuandika kwa Herufi Hodari:D

Masalkheri - salamu sa asubuhi
Sabalkheri - salamu za jioni
Treasury Bill - hati ya serekali

Sivyo kaka.

Mende au kombamwiko.

Hapo sawa.

Wacha nijaribu hii kwa vile sijaona yeyote akijaribu…
v) Kifaa maalum kwa ajili ya kuleta ubaridi wakati wa joto(fan) huitwa…
Pepezi ama ni Pepeo sina uhakika. Wakwasi saidieni

Jaribio zuri.

Uhuntha!!..sijataja mtu!

Umekosea!

Neno masaalkheyr, asili yake kiarabu!

Idhan, masaul maana yake =jioni!

Masaalkheyr=jioni njema!

Kaka, upoo?

Occurrence Book i.e OB = ?