Baada ya muda usiopimika,
Baada ya kuzuru sehemu mbalimbali kwenye ulimwengu huno,
Baada ya kutaadhmini na kuyastaajabia mandhari tofauti,tofauti,
Baada ya kuzikabili kimasomaso shughuli zilizobidi,
Baada ya kuimarisha ngome yangu ya lugha ya kiswahili kwa kuongeza ufasaha, ufahamu na umaahiri,
Baada ya kupigwa butwaa na lugha ilivyoborongwa na wale wa ’ yaliyondwele sipite’,
Mimi ndiye huyo Mwalimu nabisha tena kwa moyo mkunjuuufu…hodi hodi ‘tumesija’.
Salamu za dhati kwa ndugu zangu kina @123tokambio ,@The_Virus , @Meria Mata , @gashwin , @Mjuaji , @vincelly , @admin , @Mkufuu , @bababibitoto , @coldpilsner na wengineo wapenzi wa lugha. Kwa wageni waliojiunga nasi, dumisha umakinifu wa lugha! Na siyo tafadhali!
'Mwenda tezi na omo, marejeo no ngamani. Kijiji ni ‘ngamani’!
Sijui kwa nini naskia tu ku-derail hii thread. This village offers various eye cleansing services.Whats your take on this?
[ATTACH=full]119555[/ATTACH]