Habari zenu wakuu? Kuna hii kauli upo ugenini halafu unasikia wenyeji kuna kitu hawakioni halafu wanasema kauli hizi “Humu ndani hakijawai potea kitu” au “Hapa kwetu hakujawai ibiwa chochote” halafu mkuu wewe ndio una siku tatu tu na mgeni ni peke yako.
Iliwahi nitokea Mkuu, Hiyo ilikuwa ni asubuhi zilipotea pesa tsh laki sita lakini mpaka kufika saa 12
Zikaonekana. Siku iliyofuata nikaaga ingawa nilipanga kukaa mwezi mmoja tu. Siku 6 zilinitosha.
Mie niliwahi kuishi nyumba moja na warembo kadhaa. mmojawapo alikuwa na ndoa. huyu mwenye ndoa siku moja anaoga akavua pete akaweka juu ya madumu ya maji yangu(alivyodai).mie nimerudi late nite nikamimina maji yangu nikaoga. Asubuhi yake ilikuwa weekend nimeamka saa nne hivi nikakutana na swali kama jana nilivyokuwa namimina maji niliona pete…dah afu mrembo mmoja akachombeza lakini hapa vitu huwa havipotei…mzee nilikuwa kama nna siku kadhaa khaaaa…
hahaa au ile mtu kaingia chooni unaskia " jaman nan huyu tena mbona hii tabia ya kunya juu haikuwepo" hahaaaa my friend hata kama ulikua unaangalia world cup ghafla mwenyeji akikuuliza nan kafunga goli utashangaa unapayuka TBC1.
Na furahi kupitia ma comments za wa Tz humu kimya kimya nakumbuka enzi zangu nikiwa chuo kikuu kuna mitaa inaitwa Karen huku Nairobi kuna university imejaa wa Tz utadhani upo bongo.