Yale mambo yaliyotufanya tuwapokee wakimbizi toka nchi jirani ndiyo yametufanya na sisi tuwe wakimbizi wa mtandaoni. Tumo Kambini tunapewa msaada unaotuwezesha kuishi angalau kama binadamu mtandaoni. Asante Kenyatalk kwa kutufadhili!
Tunajiita “Diaspora”
Hii ni aibu kubwa sana kwa nchi yetu
Awamu ya 5 chini ya kiongozi jiwe ameleta utumwa wa aina yake kabisa
Hivi JF ndio mekufa? Naona umehama na jina lako, unafanyaje>
Tumekuwa wakimbizi ghafla
Kisiwa cha Amani ati8i
Jf haijafa mkuu ndio wako kwenye harakari za kuirejesha hewani, ila sijui kama itakujakuwa huru kama awali
Sijahama na jina mkuu, ila nimesajili id ile ile ilioko jf tz
Nimekupata, kweli tumekuwa wakimbizi, tumekimbia kwetu JF na kuja Kenya talk. Nina imani JF watarudi tu! JF ni maisha ya watu, kuna watu mkate wao ni JF.
Basi ngoja nami nisajiri ID yangu!
Inasikitisha sana…
Ni sawa na kutokua na uhuru au kauli mbele ya baba yake, kwa hiyo matatizo yako yote unaenda kuyasemea kwa baba wa jirani…
Hii inapelekea jirani kutambua udhaifu wa baba yako na namna gani ya kumvuruga…
Cc: @Mahondaw
Kurudi itarudi kikubwa tuwe wavumilivu tu
Wakimbizi oyeeeee!! mko nchi jirani kwa sasa mmekimbilia kisiasa
Uvumilivu ukizidi hata mbivu unaeza kuta zimeharibika ushindwe kuzila.
Ni kweli lakini tujitahidi tu kuvumilia
sisi ni watu wa kuvumilia tu. hata Melo nae huko aliko anavumilia. Acha nile Githeri akili ikae sawa
Karibu sana mkuu.
Siku zote Plan B ni muhimu katika kufanya jambo
Njoo tukutane hapa F2000 mkuu, japo ni pa kizamani ila upande huu wa stripplers utatufaa
Ni wapi huko mkuu?
Hapa Nairobi karibu na ilipp Kencom