Twende moja kwa moja. Tenga kitimoto yako na maji na tia chumvi, wacha ichemke hadi maji yaishe.
maji yakiisha anza kuigeuza geuza ili isigande kwenye sufuria. unaweza weka pilipili kwenye stage hii. endelea kugeuza mafuta yatatoka kwenye mafuta yake(stake tupu haifai).
Geuza hadi iwe ya kahawia, mafuta yake yaliyotuna inabidi uyaminye.
Mimi huwa nachemsha kitimoto na tangawizi kikishaiva…nachukua supu nagonga(nainywa) tena supu ni tamu sana,kisha hiyo nyama naiacha jikoni ikauke halafu naweka mafuta haya ya kawaida naacha ijikaange hadi ikaribie kuwa kahawia kisha naweka vitunguu maji na thaumu halafu naongeza nyanya za kawaida baadae kidogo naweka tomato paste naendelea kukoroga hadi inatengeneza rojo halafu naweka mbogamboga naendelea kukoroga nikishaona mboga zaimeiva naweka ndizi zilizorostiwa au chips au magimbi mekundu yaliyochemshwa…nikishaona ile rojo imeshaanza kukolea kny hizo ndizi au chips naipua tayari kwa kula…hii kitu inaendana na bia,k-vant,konyagi hata mbege siyo mbaya.
Hiyo kitu kuna jamaa yangu ni mtaalamu wa kukiandaa ngoja nikipata nafasi nitambelea anielekeze namna ya kukiandaa manake kisusio cha kitimoto nikitamu kuliko kitimoto chenyewe.