Kiswahili Endelevu

vinjari au kujivinjari ni kitendo cha kustahereka… hivyo kiswahili sanifu cha neno browse ni PERUZI

[SIZE=6]hujumaa, [/SIZE]@123tokambio ali gugu

nawewe umetoka wapi, hebu pewa kiti kwanza , your perusi comes from peruse

Vinjari ndilo jina mwafaka kakangu mwanakijiji mchanga.

ha haa…kuna vile hilo “neno” lilikaa nalijua lakini lilikuwa laniponyoka…nafikiri nahitaji rikizo ya dharura…ubongo umechoka.

Hehehe…hapana kaka… Kama niligugu ningetoa majibu mara moja. Hio rukwama niliisikia kwa mara ya kwanza nikiwa shule ya upili kwenye kitabu ‘siku njema’, na tokea hapo sijawai sahau…

Kuna mazoea ya kuswahilisha majina moja kwa moja kutoka kwa lugha nyingine na wakati yanatumiwa na watu wa kikundi kimoja kwa muda haimaanishi kuwa ni sahihi.

Hehehe! @123tokambio usivinjari kwenye mtandao.

Kujivinjari(kitendo cha kujitendea) pia vilevile humaanisha kujipumbaza ama kujistarehesha. Lakini vinjari ya mtandao ni kitendo cha kutenda.Kwa mfano huwezi sema najivinjari kwenye mtandao kwa sababu ukisema hivyo utakuwa umebadilisha maana ya lile ulilokusudia na kuleta maana nyingine. Tunafaa kusema navinjari mtandao.(Am browsing the internet).

Sijavinjari kaka…labda ikizidi. Kuna kitabu nilinunua; wenye kukiuza waliuza bei ya kutupa nikashuku ni wale majamaa wanaonakili bidii ya wengine. Lakini kina mengi ya kujifunza.

hakuna kuswahilisha wala kusanifisha maneno ya lugha nyinginezo bali kiswahili pekee ni lugha ya kibantu lakini iliyochanganyikana na lugha zinginezo kama kiarabu , kireno , kihindi na nyinginezo hivyo, usishangazwe na upatikanaji wa maneno ya lugha nyinginezo katika kiswahili…

REJEA HISTORIA YA LUGHA YA KISWAHILI…

KUPERUZI ndilo neno sahihi na linalotumika zaidi … yaani kuperuzi tovuti ama mtandao na si kuvinjari mtandao …

labda una mantiki yako lakini ningeomba kujua kuwa unatumia kamusi ipi ???..

Hehehehe…
Wacha utani kaka. Maneno kama tovuti, vinjari au hio ‘KUPERUZI’ hayana historia wala maana bayana, sababu kuwa yamefanyiwa utohozo tu. Hivyo basi ukisema kwamba ‘vinjari’ sio neno sahihi la ‘browse’, je neno ‘surf the web’ utasema maana yake kwa kiswahili ni?
Kadiri tekinologia inavyozidi, ndivyo pia maneno aina mbali mbali yatakavyozidi kutohozwa au kutoholewa (sijui lipi sahihi).

Twaweza jadili mpaka jua litue. Nina kamusi kadhaa na si moja kwa hivyo utafiti wangu ni wa upeo mkubwa kiasi. Kama ulivyoelezwa na @123tokambio ,majina mengi ambayo yamekuja na teknolojia(nimetohoa kutoka kiingereza) ya kisasa hayakuwepo zamani hizo. Nakubaliana nawe kuwa historia ya zama ya Kiswahili inahusisha hizo lugha ulizotaja;lakini kumbuka kwamba Kiswaili bado chazidi kukua kwa kila hali ndiyo maana majina mapya yaendelea kuzaliwa. Kwenye dhana hino, utapata majina zaidi ya moja yakimaanisha kitu kimoja.
Katika Afrika Mashariki, tuko na Chama Cha Kiswahili kinachoshughulikia kuyasahihisha na kuhalalisha maneno mapya katika lugha ya Kiswahili. Chama hiki kinahusisha walimu wa vyuo vikuu na weledi watajika wa kiswahili kutoka Kenya na Tanzania.

ahsante kwa kujua kuwa huu ni mjadala mrefu sana kwa kuwa lugha ni suala pana…

kutohoa misamiati ya lugha nyinginezo haiondoi usanifu wa lugha husika kwa kuwa kuna lugha kama kiswahili ina uhaba wa maneno ya kisayansi hivyo, kutohoa misamiati ya lugha nyinginezo hakuepukiki…
hii ni tabia ya lugha nyingi duniani ukijumuisha kiingereza

nashukuru kwa mchango wako uliojaa utaalamu wa lugha hii ambayo kwangu ni lugha mama pia …niliisoma hadi shule ya upili pekee

salutee