-Mouse (ile ya tarakilishi au kipakatalishi) huitwa puku au kipanya.
-Website ni tovuti.
-Internet ni Mtandao.
-Browse ni vinjari na kadhalika na kadhalika.
N/B.Twashukuru maulana, muumba wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo kwa kutuwezesha kuiona Jumapili nyingine. Waja wa dini ya kikristo ni siku nyingine ya kumuabudu Jalali.[/B]
Asante Mwanakijiji Mkuu Bw @xuma
Kutoka leo sitochanganya matumizi ya maneno ‘tovuti’ na ‘mtandao’.
Kwa sababu mimi ni Mkenya halisi siwezi tafsiri hayo maneno bila usaidizi wake Google.
i) Hiccup…Chechevu/Kekeru/Kikwifukwifu/Kitefutefu/Kwikwi. Hongera @4makind ind kwa kupata jibu sahihi.
ii) Apple…Tofaa au Matofaa kwa wingi. @emali , kongole kwa kupata hili.
iii) Appliance…Ala au kwa wingi Nyala
iv) Gadget…Kidude au Kifaa. Kongole @Meria Mata, na @weston kwa kung’amua hili.
v) Forum…Ukumbi au jukwaa lakini jina jukwaa mara nyingi humaanisha ‘stage’. @Weston na @emali kongole.
vi)Handcart…Rukwama. Kongole @123tokambio kwa jibu sahihi.
@kender9 [/B]Shukran kwa kushiriki japo hugugonga ndipo.
Nawaacha na msemo ‘Mfa maji haachi kutapatapa’.