Sadakta! Tumakinike tena kwenye ulingo huu wa lugha yetu tunayoitukuza. Leo tutaangazia makosa ambayo yame’boreshwa’ kwenye maongezi ya kileo mpaka kiswahili kinaborongwa na kuharibiwa kwa upeo mkubwa! Makosa hayo yamebuka kuwa mengi na hatuwezi kuyaangazia yote japo kwa kiasi fulani kwenye kila fursa.
Makosa ya usemi wa kileo:
-Ni makosa kutimia kiambishi 'ju’ ukikusudia kumaanisha 'kwa sababu’. Kwa mfano ni makosa kusema ‘Nimechelewa ju nililala sana’.
Usahihi ni kutumia maneno; Kwa ajili, kwa sababu, kwa kusudi, au kwa minajili. Kosa hili limekidhiri sana kwenye kizazi cha sasa.
-Hatutazami na macho bali tunatazama kwa macho.
-Hatusemi ‘Mtu mgani?’ Twasema ’ Mtu yupi?’ Neno ‘gani’ ni kiambishi tasa na hakiambatanishwi na kivumishi chochote haswa tukielezea juu ya Mtu au watu. Mfano kama huu tena ni twasema ‘Mwanafunzi safi na wala siyo Mwanafunzi msafi’.
-Neno 'mnene’ hutumiwa tu kwa mwanadamu kwa mfano ’ Juma ni mnene kuliko Jese’. Nano ‘mnono’ hutumiwa tu kuashiria wanyama.Kwa hivyo likitumiwa kuashiria mwanadamu ni matusi.
Kama nilivyoeleza hapo juu kwenye mfano was Juma na Jese, uyaona nilivyowafananisha. Hatusemi 'Juma ni mnene kumliko Jese bali twasema Juma ni mnene kuliko Jese.
Tutaliendeleza hili somo kwenye sehemu yake ya pili katika vipindi vijavyo.
CHEMSHA BONGO
-Hawa ndege waitwaje kwa kiswahili?
i) Peacock…
ii) Flamingo…
iii) Guinea fowl…
iv) Honey bird…
v) Heron…
vi) Wood Pecker…
vii) Falcon…
viii) Eagle…
ix) Jiko la makaa huitwa aje kwa Kiswahili?
x) Pulpit ni nini kwa Kiswahili?
Hayo ni maswali mboga kabisa kwa Leo. Jikakamueni.
Msemo wa Leo. Mchimba kisima huingia yeye mwenyewe!
MAJIBU YA LEO:
CHEMSHA BONGO
-Hawa ndege waitwaje kwa kiswahili?
i) Peacock…Tausi. Kongole @Nottybwoy , @Mjuaji ,@TerribleWaste na @Chifu
ii) Flamingo…Heroe
iii) Guinea fowl…Kanga. Kongole @TerribleWaste , @Mjuaji na @Chifu
iv) Honey bird…Keremkerem
v) Heron…Koronga
vi) Wood Pecker…Kigogota
vii) Falcon…Kozi
viii) Eagle…Tai. Kongole @TerribleWaste
ix) Jiko la makaa huitwa aje kwa Kiswahili?..Seredani
x) Pulpit ni nini kwa Kiswahili?..Mimbari. Kongole @TerribleWaste
Maswali ya Leo yamekuwa kizungumkuti kwa wengi lakini natumai tumejifunza mapya. Kongole kwa wale wote walioshiriki na waliochungulia dirishani kama kina @4makind , @vuja de ,@sludgist , @introvert ,@jumabekavu na wengineo. @123tokambio kwani Leo uligonga ukuta?