Manchestes United(Red Devils) Special Thread.

Shunie naww ni Man u

mkuu kim naona trump kakubinya makende…

Ni man u mkuu

mods umrekebishsha heading afu umekosea please naomba usahihishe

Tetesi

Duh i miss the origino red devils special thread

@Shunie mwambie afanye mambo

I cant wait kuwaona fred na dalot pale OT

Naona jukwaa letu mods na victor wameshindwa kabisa kulirekeisha

Mabingwa wa Ligi ya Premia Manchester City wataanza msimu kwa mechi ya ugenini dhidi ya Arsenal wikendi ya 11-12 Agosti msimu mpya wa Ligi Kuu England utakapoanza.

Arsenal wataanza msimu wakiwa na meneja mpya Unai Emery aliyemrithi Arsene Wenger, Mfaransa aliyeondoka klabu hiyo baada ya kuwa kwenye usukani kwa miaka 22.

Tottenham watasafiri Newcastle kisha wacheze dhidi ya Fulham katika uwanja wa Wembley wakisubiri uwanja wao mpya unaogharimu £850m umalize kujengwa.

Manchester United watakuwa wenyeji wa Leicester City, Liverpool nao wakutane na West Ham, huku mabingwa wa Championship Wolverhampton Wanderers wakialika Everton uwanja wao wa Molineux.

Fulham waliopandishwa daraja watakuwa wenyeji wa Crystal Palace, huku Cardiff wakiwazuru Bournemouth.

Chelsea watasafiri Huddersfield, Southampton wawe wenyeji wa Burnley, nao Watford wakabiliane na Brighton uwanjani Vicarage Road.

Mechi za wikendi ya kwanza

Arsenal v Manchester City

Bournemouth v Cardiff City

Fulham v Crystal Palace

Huddersfield Town v Chelsea

Liverpool v West Ham United

Manchester United v Leicester City

Newcastle United v Tottenham Hotspur

Southampton v Burnley

Watford v Brighton

Wolverhampton Wanderers v Everton

De gea asaini mkataba wa miaka 5 man utd
[ATTACH=full]176453[/ATTACH]

Hivi Huku Duniani Kuna Degea Wawili?
Yule Wa Jana Wa Spain nahisi Ni Photocopy Wa Yule Wa Man United.
Nadhani Yule Wajana Ni Mdogo Wake Karius.

[ATTACH=full]176650[/ATTACH]

Ronaldo mwanga Yule

Yupo mmoja.

Ila huwa hafanyi yale makosa akiwa na man untd…!

na morinyo soon anampa mkataba mpya

And that is what we 'll like to witness.

Manchester United imekamilisha usajili wa Kiungo wa Brazil Fred kwa kitita cha pauni 47.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye anaiwakilisha Brazil nchini Urusi Kombe la Dunia, anajiunga na klabu hiyo kutoka Shakhtar Donetsk.
Amesaini mkataba wa miaka mitano.
Ni mchezaji wa pili kusajiliwa na Kocha Jose Mourinho kufuatia uhamisho wa Diogo Dalot kutoka FC Porto.
“Hii ni klabu bora duniani na ni furaha kubwa kujiunga nao,” alisema Fred.
“Kufanya kazi na Jose Mourinho, ambaye ametwaa mataji mengi akiwa mkufunzi, ni fursa muhimu.”
Mourinho amesema: “Fred ataongeza ujuzi kwenye kikosi chetu cha viungo wa kati, ujuzi unaohitajika; ubunifu wake na maono wakati wa kutoa pasi vitatupatia sura mpya kwenye uchezaji wetu.”

Fred ameiwakilisha klabu ya ligi kuu ya Ukraine ya Shakhtar ambapo aliisaidia kubeba mataji ya ligi kuu mara tatu, kombe la Ukraine mara tatu na mataji manne ya Super Cup Ukraine.
Alijiunga nao kutoka klabu ya Internacional mnamo 2013 na kuwafungia mabao 15 kwenye mechi 155.
Msimu uliopita, Fred aliisaidia Shakhtar kufika hatua ya muondoano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Fred alishiriki kwenye ushindi wa Shakhtar dhidi ya Manchester City na Napoli, na kufunga goli dhidi ushindi wa 2-1 dhidi ya Roma hatuaya 16 bora.
Kufikia sasa Fred hajashiriki Kombe la Dunia licha ya kuwa kwenye wachezaji wa akiba dhidi ya Uswizi.
Mechi hiyo ya ufunguzi ilikamilka sare ya 1-1.

Wakuu huyu Lukaku inabidi atafutiwe watu wa maana pale utd.Kwa kweli tulilamba dume,huyu ni bonge la striker

halafu kabadilika sana chini ya mtaalamu th14 vavavuuuuum

Nipo hapa shetani mwekundu
Nalog off