Only people who have worked at a mujengo site can relate

Kazi mbaya ni ya kupandisha mawe… kupandisha mawe moja first floor ni 2 - 3ksh kabla umake chapaa ya msee mkono itabidi umebeba mawe 300.

Watu wale wa lumberjack saw kabla powersaw ziwe common ndio niliona walikuwa wanakula sana huko western. Gorogoro moja wanakula wawili au watatu na omena au mboga kienyeji.

Nilienda kudai pesa ya simiti nimepandisha foreman akasema niiteremshe…mimi ni nani…nikateremsha nne lakini,mgongo ikaanza kuuma tena.Hapo mimi na kiraikoo tukapeana heshima…

Na bado hukulipwa?

Wapi,alisema analipa mtu amemaliza siku

wale wa shimo ya coronge ndio iwekwe baruti walikuwa pure muscles,imagind drilling a 12 ft or more kupitia kwa mawe using tarimbo mrefu?

inaonekana majority ya nyinyi ni watoto wa masonko,kazi ngumu hakuna anaye ifanyia kupenda,kama hamujawahi kubeba simiti ikiwa moto hakuna kitu mnajua ama kuoffload mchanga ya miguu kumi ya single diff,ukirusha karibu ifungie miguu kidogo hio lori haitoki hapo na saa hio uko solo

:D:D huyu ni kama hayuko Kenya sio eti hawezi afford chapo ya kinde.

ni kusema kula ako hakuna wheat flour?

Maybe wapishi ndio hawako.

Lorry ya miguu kumi ya single diff? hio ni ya axel za 6x2. Kazi ngumu ndio ziko na quick cash hapa Kenya na wengi wanazitaka, kwa hivyo supervisors hujigamba sana. Kitu muhimu sasa ni mechanization iko more effecient.

One of true Kenyans wako kwa trump na hawatingi kama kina nani hapa ktalk.

wewe ni mwingine

True this. Kuna siku beste yangu alinipeleka job ya relief maize pale Transami Warehouse Embakasi, tulikuwa tunalipwa kwa zile gunia umepandisha huko juu at the end of the day. Niliambiwa siri ilikuwa kuangalia foreman na macho za huruma na machozi kama umeshilikia mashavu na mkono moja ndio uchukuliwe kibarua. Well, it worked and we were both let in since he was a veteran.

Yaani ulikuwa unapanda na gunia mbio ukifika 4th step unaskia bone murrow zimeisha kwa magoti inalia ni kama hinge ya mlango haina grease na saa hiyo uko supposed kwenda mpaka 16th step.

Ukiangalia time ni saa nne na lunch break ni 1pm, saa hizo Wakaba 1GB wa pipeline wanapanda wakishuka kama Marcelo akichezea Real Madrid unashindwa wewe uko na shida gani na wewe ni weider.

I was paid that evening, bought a bottle of Kaluma balm the balance nika nunua mguu ya ng’ombe (Firestone), supu ya pilipili na ugali. Then nika peleka mabeste kwa mama Scola (kwa Getty) nikawanunulia chang’aa nikiwasimulia hekaya.

Sikuwahibrudi huko tena…

…hao watu wako ni waoga sana:D:D