mwanaume anakaz nzuri kiasi ila ukoo mzima unamtegemea yeye uko kijijini baba ake anawake 3 ambapo asilimia 80% wanamtegemea jamaa kuanzia chakula kila kitu
Sasa jamaa kumbe alimpenda bidada kwakumuona anaroho nzuri pia anakibiashara kidogo ambacho kinatosha …so lengo la jamaa nikwamba wasaidizane na bidada kuwainua familia yake kiuchumi
Sasa ugomvi unakuja maana bidada anandoto za kua na maisha mazuri angalau aweze kuishi vizuri ,wakati jamaa anania ya kuwainua kwao ikiwemo kuwasomesha kuwajengea
Bidada kaniomba ushauri anashindwa aamue nini sababu jamaa jana kamuambia hela yake yeye anajenga na kufanya maendeleo kwao hela ya bidada inabidi atumie kwa ajiri ya kufanya maendeleo,kununua vitu vya ndani yeye atakua anamsaidia kidogokidogo,
Bidada anaona kama nimtihani mzito sababu hata mahitaji yake binafsi jamaa hayafanyi juz wameenda shopping mdada kanunuliwa kiatu cha elf 10 tu wakati jamaa katumia laki 3 kununua nguo na viatu vya ndugu zake
Hahaha sio mshamba hizo ndo familia nyingi za kitanzania zilivyo. Sasa kuna nyingine mwanaume anaoa mke ambae na anahudumia familia ya mkewe pamoja na yake
Kama ndo wewe ungeamuaje? Mbona kuna wanaume wanasaidia familia ya mke hili suala kwa mwanamke mwenye akili haliwezi vunja ndoa/mahusiano yake na mumewe
kama ni mm tungekaa tuongee mapema kabla hatujafika mbali swala la kusaidia ndugu sio shidaa …je anatoa huduma ya familia? kama hatoi ananiachia mm pekee hapa sitaelewaa
kama anabalance kote ni sawa tunasogeza maisha sabbu familia zetu za kitz ndo hvyo
Familia nyingi za kiafrika zikikusomesha ujue wewe ndiobunakuwa nguzo ya kuinuia ukoo mzima huyo mwanamke aachane nae huyo mgongo wa ukoo atamchelewesha sna maana hataki kuwasaidia wazazI ili wasiwe tegemezi kwake yeye anataka kuwabeba muda waote