Ukitembelea nzuzi mbalimbali humu Kenyatalk na kuona zinavyowasilishwa utaona kwamba hawa jamaa wana uhuru mkubwa sana wa kujieleza. Wakati mwingine Lugha zinazotumiwa na wenyeji wa Kenyatalk hukuacha mtu umeasama mdomo. Kuna baadhi ya thread humu zingekuwa kule nyumbani tayari wenyewe wangekuwa wako jela.
Nilichogundua hoja hazifutwi bali hujibiwa kwa hoja ama wakati mwingine kwa mitusi ya nguoni. Pekee ninachojiuliza kama matumizi ya matusi kwenye kujibu hoja inatokana na uchache wa misamiati ya Lugha waliyonayo wakenya ama ni kutokana na tabia walizo nazo.
Yanini sasa kufananisha nchi mbili tofauti kwa mnadhili mmoja? Hukupaswa kutambua ya kuwa kunde ni kunde na maharage ni maharage? Yakufaa nini kutaka ngano kuwa kama mahindi?
Wakati mwingine kuchanganya vitu hufanya vitu kuwa bora zaidi. Jee kugundua kwamba ngano na mahindi ni tofauti siyo hatua kuelekea kwenye ufahamu bora zaidi kuhusu vitu hivyo!?
Hivi hauoni huo ni una fiki wa ki aina.una mtusi mtu eti kwa ustaarabu ndio badae usipate lawama. unajaribu bado kuonekana kama mtu mzuri lakini cha msingi nikua ume mdhalilisha na jama atakua kesha kasirika.
Kenya hakuna cha kuficha,kama wewe mkora bora tukuite mkora na hilo liishie hapo.
Kila lugha ina kanuni zake, tafsida si unafiki bali ndiyo matumizi yenyewe ya Lugha ya kiswahili. Kwa mfano si sawa kumwambia mtu mzima wewe ni mshenzi lakini ni rahisi kumwambia kwamba wewe si mstaarabu na ivo maana yake mtu ambaye si mstaarabu ni mshenzi!