JamiiForums kurejea hewani muda wowote kuanzia sasa

JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Asante kwa kuendelea kuwa mvumilivu wakati huduma yetu ikiwa haipatikani. Tutarejea hewani muda mfupi kuanzia sasa!

Uongozi - JamiiForums

Copy & paste kutoka mlangoni mwa home of great thinkers

Wao what great news!

Safi sana ikirudi,Ila hao tcra watakuwa washajifunza kupitia kenya talk,hata wakikomaa kuifungia jf bongo lakini tushapata njia mbadala

Hilo neno “kuanzia sasa” halina deadline…Bora wangesema baada ya saa 12,24,48 na kuendelea.

Hata hivyo tunaombea iwe muda mfupi kweli… maana mule mnamadini hai mengi sana.

Ila hata ikirudi mi naona huku ndo kuzuri maana jiwe anapigwa mawe kisawasawa bila hofu ya kula ban.

habari njema sana hii…

Hili bandiko lina siku ya tatu kama sikojakosea. Muda wowote = infinity
Hata yesu/jasu/yisa tumeambiwa atarudi muda wowote kuanzia siku hile alipopanzwa, leo ni 2000yrs

Haiwezi kurudi ikiwa na ile sera yake ya Where we dare to talk openly

Tukiwa huku ugenini Ujumbe unafika kama ulivyo kusudiwa
Nafikiri jukwaa la siasa litakuwa Hai likiwa igenini kuliko nyumbani

Hilo tangazo liko lina muda mrefu na liko too general…Ntakukumbuka daima Jf

Majirani tunawashukuru kwa ukarimu wenu, karibuni TX kule tunae MK254 na Nairobi.

Nakubaliana na wewe mia kwa mia.

Mimi naona isirudi tubaki huko ugenini tuwe huru wasije kutugata kwa urahisi na kutushitaki kwa kuwa kosa limetendeka Tanzania lakini ukiwa nje ya nchi hawana ubavu Wa kukushitaki hata kama wanakuona

Irudi tu ula hata ikirudi nahisi itakua tofauti kabisa watakua wamebanwa.
Tutaendelea kubaki huku kama mbadala

Mimi nitabaki hapa hapa Kakuma refugee camp

Daaah bora ugenini nishida kwakweli!!najilazimisha tu kua hapa.

watu wanashtakiwa kwenye fb,twitter na inster na vyote viko nje itakua hapo tu kenya jidanganye tu,

Naamini itakua ya ovyo tu…uhuru utakuwa umepungua,na moderator watakuwa wanaachia nyuzi za chitchat na MMU huko ndo ziwe active

Tuwe wavumilivu kama watarudi chini ya masharti magumu tunaliendeleza hukuhuku

Kuzuia uhuru wa habari kunakunufaisha nini wewe hata ufurahie?