JamiiForums kurejea hewani muda wowote kuanzia sasa

Watu wanaouchukia ukweli Huwa na matatizo kwenye ufahamu wao.

Ni sawa na ban za masaa kadhaa kule JF,mtu unaweza dhani ni masaa matatu manne kumbe masaa kumi na mbili. Tuwe na subira tu

Mimi pia sirudi Tz. Huku pazuri…hakuna ban zisizo na msingi pia mods wa kenyatalk ukiwapm wanarespond haraka kuliko jf unajibiwa baada ya miaka mitatu.

Basi tutakuwa wote hapa tukipeana company

Poa poa ndugu yangu.

Asante tulishaanza kuzoea huku Kenya

hivi inawezekana akahamishia kampuni kenya??

Wakenya sio huku mitandaoni tu, kwenye kila huduma customer care wako vizuri. Huko Tz unakuta mtu wa customer care anaongea na simu mambo yake binafsi mpaka amalize ndio akusikilize. Kwetu Tz ni shida huo ndio ukweli wandugu.

Basi tunaobaki tujiandikishe:D. Ila nadhani kulikuwa na makubaliano confidential kati ya KT na JF watuwekee hili jukwaa hapa. JF ikirudi litatolewa. Labda tuanze kulobby watuwekee jukwaa la watanzania KT.

Hahahahhahahh!

Warudi tu; kijijini panachosha

Hata wakitoa jf huku mi nitaendelea kuwepo. Ila watuachie angalau jukwaa moja maalum kwaajili ya watanzania, kama ambavyo JF ina jukwaa linalohusu wakenya

Lakini mimi nimepapenda sana huku, kwanza hali ya hewa ya huku si sawa na ya kule! Kilichonivutia zaidi ni ukarimu wa Wakenya, jamaa ni wakarimu sana.

Mi mwenyewe nimefurahia uhuru wa kulipasua jiwe lenye nundu sugu ya uzinzi.

MImi mpaka niwe waziri kama Joseph Misri ndio nitarudi.

Mkuu kulipasua jiwe ni jambo dogo sana. Tunapaswa kujadili mambo ya msingi hata watu wengine wakiangalia wajue tuna hoja za msingi. Tukiishia kulipasua hilo jiwe kwa lugha za kejeli tutawapa watetezi njia nyepesi ya kukwepa hoja zetu kwa kusema lengo letu ni kutafuta uwanja wa kutukana na sio zaidi.

Sawa mkuu nimekuelewa.

They have come to their sense and realised that they cannot withstand insults hurled to them from this end. shame on those fools out there

Wakitaja siku itakayorejea itakua vyema zaidi

Aaah, wewe mkuu umeishia Kakuma? Mimi maisha ya pale yalinishinda nikaoitiliza mpaka huku Mboloni Refugee Camp!