JamiiForums kurejea hewani muda wowote kuanzia sasa

Hahaha hapa kakuma kuna faraja sana huwezi kufa njaaa

Mods wa JF walikuwa wameharibika sana, ulikuwa ukiligusa jiwe tu unakula ban! Walikuwa wameanza Kutafsiri nyuzi kama policcm! Wakihisi tu unalizungumzia jiwe unalamba ban!

itakuwa poa ikirudi maana kuna madini hasa biashara na kilimo

Hilo tangazo lina muda kidogo…

Cc: @Mahondaw

numbisa ila humu sitoki mpaka mkeii mmoja aliwe

Sijajua kama, Jamii Forum ikirudi na mada izi tulizojadili zitapatikana au ndio kwenye savers zao hazitaonekana

Tukirud tz uhuru wakuandika utakuwa haupo tena,madmin watakuwa wanazitoa zote mbaya

Tutapigs miguu yote bando letu wasituchagulie pa ku surf

:D:D:D:D:D

Irudi tu tutakuwa na uraia wa nchi mbili

kweli kabisa tena itakua vyema aise.

Kurudi sawa ,ila isiwe ndio wamekabidhiwa key ,tcra

Upande wa jukwaa la siasa halitokuwa huru tena kama awali maana tisiaraei wameweka sheria ngumu sana kwa wapashaji habari za ufisadi ambao utapaswa kuelezea chanzo chako cha habari

Na kwa mantiki hiyo nafikiri hata jf ikirejea nashauri jukwaa la siasa kule lifutwe ila mambo yote ya siasa yahamishiwe huku ughaibuni tuendelee kuibana serikali ya mfalme juha ili iongoze kwa kufuata katiba na siyo mawazo na maamuzi ya kijinga kimoja na kishoga chake.

Hata ikirudi sisi wengine tutabaki humu humu. kwa maana huku pana uhuru zaidi.

Nionanvyo mimi ikirudi itakuwa kama kuku aliyetolewa manyoa yote na kuachowa atembee au ni kama simba aliyengolewa meno yote.

Tangazo lenyewe:
Asante kwa kuendelea kuwa mvumilivu wakati huduma yetu ikiwa haipatikani. Tutarejea hewani muda mfupi kuanzia sasa!

Uongozi - JamiiForums

Tunaofuatilia, hili linaonekana lina matumaini zaidi.

Uhuru utakuwa umebinywa sana sana

Hilo Tangazo Lipo hivyo tokea Jana Asubuhi. Nashindwa kuelewa ‘‘muda Mfupi tokea sasa ni Saa ngapi?’’

Lina muda hlo tanganzo maana hawatoi taarifa kamili

Basi kama ni hivyo so wakweli. Muda mfupi ujao should not exceed one hour… umezidi basi ndani ya saa sita