Baada ya Superstar Richmavoko kutoonekana kwa kipindi kirefu katika camera za WCB, na kutotoa nyimbo mpya kwa mda mrefu, Tetesi za chinichini kutoka kwa watu wao wa karibu inasemekana Rich mavoko na Bosi wake Diamond Platnumz kwa sasa wamevurugana
Tetesi zaidi zinadai kwamba Mgogoro uliazia wakati Diamond akihitaji Rich Mavoko ampe nyimbo yake ya Rudi aliyomshirikisha Patoranking lakini inasemekana kuwa Rich mavoko alikataa kumpa Diamond Platnumz hiyo Nyimbo, ndipo Vuguvugu la kutoelewana likaanzia hapo
Inasemekana baada ya Mavoko kukataa kumpa Diamond nyimbo ya rudi ili aiimbe yeye, ndipo Mavoko Akaanza kutengwa kimya kimya
Dalili zilianza kujionyesha pale Crew nzima ya WCB ikiachia nyimbo mpya kila baada ya mwezi , lakini mavoko hajatoa kazi mpya kwa mda mrefu hadi mashabiki wakaanza kumshambulia kwa maneno makali kwenye Account zake za Instagram na Twitter bila kujua nini kinaendelea, hata kwenye events na show za WCB Rich mavoko hakuonekana kwa kipindi kirefu, hadi sasa Mavoko haonekani kwenye events yoyote ya WCB
Rich bana alitakiwa nae awe mtu wa majungu na kiki Mbuzi kama watu wa wcb ila sasa jamaa mpole anawaza kazi zake tu. Rayvanny anaenda nao hivyo hivyo sababu anajishusha sana ili mradi asikose pesa ya kulea mwanamke wake
Sana hana msimamo. Mtoto anateseka kwa makosa yake,tununu na mama dai. Hao wana ugomvi bora wakae waombane msamaha yaishe na sio kuleta visingizio na kutukana timu walizozianzisha wao wenyewe
Nahisi keshafutwa au anaondolewa mdogo mdogo maana ajali aliyoipata ni kubwa sijaona boss akienda mtembelea hosp na picha juu kama kwa zama alipojifungua
Kiki kwa pikipiki,kama diamond alikuwa anataka wimbo wa mavoko si angetangaza dau tu,hivi msanii hawezi kufanya promo wimbo wake mpaka atengeneza “KIKI”?
Kingine tale na salam wameshaanza kujiweka kando kiaina au labda wameamua kupunguza mazoea binafsi na dai na kuweka mbele mazoea ya kazi baada ya kuona kijana haeleweki kama zamani